Entertainment

Harmonize atangaza ujio wa wimbo mpya kuhusu wapenzi wa zamani

Harmonize atangaza ujio wa wimbo mpya kuhusu wapenzi wa zamani

Mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize ametangaza kuachia wimbo mpya Ijumaa hii, kueleka siku ya kutoa wimbo huo,

Kupitia Insta Story yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize ametoa ufafanuzi kuhusu wimbo wake mpya unaotarajiwa kutoka, akisisitiza kuwa hauhusiani na mpenzi wake wa zamani.

“HAIHUSINI NA X WANGU YEYOTE!!! NINA HESHIMA KUBWA SANA KWAO WOTE.”, Amesema Harmonize.

Kiongozi huyo wa konde gang ameeleza kuwa hawezi kuimba kuhusu mpenzi wake wa zamani, kwa sababu heshima na upendo wake kwao umebadilika na kuwa wa kifamilia.

“KAMA NIKIMUIMBAJI X WANGU YEYOTE HAITOKUWA KAZI KUBWA KAMA MNAVYO DHANI! ILA NDO SIWEZI UPENDO WANGU UNAUPITILIZA NA KUWA KAMA KAKA MDOGO KWENYE FAMILIA.
SO HATA TIKTOKA TUMESHINDWA HESHIMA NA ADABU YANGU KWENYE FAMILIA INABAKI PALE PALE, SO HATA AKINIUNIKA TUNAKUTANA KWENYE VIKAO VYA FAMILIA 😂.” Ameeleza.

Pia, ameongeza kuwa wimbo huu ni kwa niaba ya watu wote walioachana na wapenzi wao, sio maisha yake binafsi pekee.

“HIZI GOMA NI KWA NIABA YA XXX WOTE DUNIANI, MSINIPENDE KUAONA MNAYAWATA WAKWENU TUU KISA NIMEMBA MTE 😂 SEE YOU ON FRIDAY KUMEKUCHA!!!”, Ameongeza Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *