
Staa wa Muziki nchini Tanzania Harmonize ametoa ufafanuzi kuhusu Tamasha la Afro East Carnival msimu wa pili.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram harmonize amesema Tamasha hilo linalotarajiwa Kufanyika Mei 29,mwaka 2022 katika Uwanja wa Uhuru,jijini Dar es salaam hakutokuwa na Wasanii waalikwa kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la kwanza alilotangaza List ya Wasanii waliomsindikiza.
Harmonize amebainisha kuwa hii ni show yake na wanaopaswa kuhudhuria ni mashabiki wake tu.
“Hii ni show ya Konde Boy wanaopaswa kuhudhuria ni Kondegang F.C tu.” Β ameandika Harmonize kupitia Instagram.
Lakini pia staa huyo Amesema katika Tamasha hilo atatumia Masaa 4 jukwaani na atatumbuiza nyimbo 60 huku akisema kutakuwa na Suprise nyingi ambazo hazitotangazwa