
Msanii wa Bongo Fleva Harmonize amewashauri wasanii wenzake wapunguze kuimba nyimbo za pombe hasa mwezi huu wa januari.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema sio watu wote wanakunywa pombe ila nyimbo za kuhamasisha pombe zimekuwa nyingi sana.
“Wasanii punguzeni nyimbo za pombe..msidhanii hii nchi kila mtu ni mlevi..Hata tunaokunywa juma 3 hatunywi tukizisikia nyimbo za pombe kama unatonesha kidonda!!! Hasa hasa JANUARRY hii”, Aliandika Instastory.
Kauli hiyo ya mtu mzima Harmonize imeonekana kuzua hisia kinzani miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo msanii mwenzake Rayvanny amelazimika kuingilia kati mjadala huo kwa kumtaka bosi huyo wa Konde Gang kukoma kuzungumzia masuala ambayo hayamhusu.
“Huna Ngoma ya pombe uliowahi ku hit sasa utaongea nini kuhusu pombe shut the f****ck up #NITONGOZE VIDEO COMING SOON”, Aliandika instastory.