Entertainment

HARMONIZE AWATOLEA UVIVU WANAOPINGA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA

HARMONIZE AWATOLEA UVIVU WANAOPINGA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize amesema atashiriki kwenye Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) licha ya kuwepo malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu.

Akizungumza kwenye One Love Concert Harmonize ameitaka serikali kutokatishwa tamaa na maneno ya watu kwani hata tuzo kubwa za nje zimekuwa zikilalamikiwa kwa sana.

“Kama umeliona jina langu basi ujue nitashiriki kwa asilimia 100, kila mtu ana haki ya kusema kile anachojisikia kwa sababu hata tuzo nyingine ambazo tunaweza kusema ni bora kuliko tuzo za nyumbani zinalalamikiwa siku zote” amesema Harmonize.

Utakumbuka tuzo za muziki nchini Tanzania zinarejea baada ya miaka saba tangu kusitishwa kwa Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) mwaka 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *