
Staa wa muziki wa Bongofleva, Harmonize anaendelea kuweka wazi matamanio yake ya kumfanya aliyekuwa mpenzi wake Kajala Frida kuwa Meneja wake akiamini kuwa kufanya hivyo kutaongeza kitu kwenye uongozi wake kutokana na akili yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram harmonize amesema kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu ataacha kujihusisha na majukumu ya biashara ya muziki na kumwachia mpenzi wake, Kajala.
Lakini pia Kajala atashirikiana na mameneja wengine waliopo nyuma yake.
Harmonize amekazia kurekodi muziki na kutumbuiza Jukwaani ndio majukumu yake kwa sasa, kisha mpenzi wake Kajala Frida atadondoa wino kwenye dili za Kibiashara.