
Wasanii wa kundi la Hart the band kutoka Kenya wamewaonya vijana dhidi ya kubugia pombe kupindukia.
Wakizungumza moja kwa moja na Mpasho, wamesema vijana siku hizi wamekuwa waraibu wa kutumia vileo bila kuchukua tahadhari, jambo ambalo wamedai kuwa ni tishio kwa usalama wao ikizingatiwa kuwa wengi usahau kula na hata kuendesha magari kiholela wakiwa walevi.
Katika hatua nyingine wamesema hawatumii ‘kiki’ kutambulisha kazi zao za muziki kwa sababu si aina ya maisha ambayo wamezoea tangu waanze muziki miaka kumi iliyopita.
Wasanii hao ambao walilamba dili la ubalozi wa kinywaji cha Black & White wameongeza kuwa aina ya mashabiki wao pamoja na kazi zao nzuri za muziki wanazotoa pia huwafanya wasifikirie kabisa masuala ya kiki kama ambavyo hufanyika kwa baadhi ya wasanii hapa nchini Kenya.