Sports news

Hatma ya James Reece kujulikana masaa 48

Hatma ya James Reece kujulikana masaa 48

Kocha wa Chelsea Graham Potter amesema hali ya majeraha aliyoyapa mlinzi wa kulia wa klabu hiyo Reece James kwenye mchezo wa EPL dhidi ya Bournemouth itajulikana ndani ya kipindi cha masaa 24 hadi 48 ili kujua ukubwa wa jeraha lake.

James alipata maumivu ya goti na kutolewa kwenye mchezo dakika ya 53 kwenye mchezo ambao Chelsea imeshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Bournemouth.

Kwa Upande mwingine kwenye EPL Usiku wa hapo jana klabu ya Manchester United ilifanikiwa kuinyuka Nottingham Forest mabao 3-0 mchezo uliochezwa Old Trafford.

Ligi hiyo inaendelea tena leo kwa mchezo mmoja Manchester City wanacheza ugenini dhidi ya Leeds United Saa 2 usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *