Entertainment

HUDDAH MONROE AJIPIGA KIFUA KUHUSU ISHU YA KUWACHAGUA WANAUME WANAOTESHELEZA KIMAPENZI

HUDDAH MONROE AJIPIGA KIFUA KUHUSU ISHU YA KUWACHAGUA WANAUME WANAOTESHELEZA KIMAPENZI

Mrembo kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe amejisifu kuwa anajua sana kuchagua wanaume ndio maana ma-ex wake huwa wanafuatiliwa sana wanawake ambao ni rafiki zake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Huddah amesema kutokana na hilo, imekuwa ni ngumu sana kwake kwa sasa kuweka wazi mahusiano yake ila hivi karibuni anaweza kujaribu kufanya hivyo.

“Kitu pekee ninchohitaji kwa mwanamume ni uaminifu na heshima, wengi wamo humu nje lakini hawana ladha, marafiki zangu wa kitambo walikuwa wanawamezea mate na kuwatafuta ma-ex wangu kwani walijua huwa nachagua vizuri”. Ameandika kupitia Instagram

Ameendelea kwa kusema; “Hii ndio sababu huwa siposti mwanamume wangu mitandaoni, kwa maana wanawake watamtamani, lakini nitamposti mmoja hivi karibuni.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *