LifeStyle

Huddah Monroe Ashukuru Wakili Aliyemsaidia Kurekebisha Meno Yake

Huddah Monroe Ashukuru Wakili Aliyemsaidia Kurekebisha Meno Yake

Mrembo maarufu katika mitandao ya kijamii, Huddah Monroe, ameonyesha shukrani zake kwa wakili mmoja wa Kenya aliyemsaidia kurejesha tabasamu lake kwa kumsaidia kifedha.

Kupitia Instastory, Huddah amefichua kuwa wakili huyo alimpatia shilingi milioni 2, fedha zilizotumika kurekebisha meno yake yaliyokuwa yameharibika baada ya kuhusika kwenye ajali akiwa bado msichana mdogo.

Akizungumza kuhusu safari yake ya maisha, Huddah amesema alikulia katika mazingira ya umaskini, hali iliyowafanya wazazi wake kushindwa kumhudumia kwa matibabu ya meno. Upungufu huo ulimfanya kukumbwa na changamoto kubwa shuleni, ambapo wenzake walimchekelea kwa kukosa meno ya juu (front teeth)..

Kwa sasa, Huddah anasema msaada huo umempa nguvu mpya na kuondoa majeraha ya kisaikolojia aliyobeba kwa miaka mingi. Amepongeza wakili huyo kwa moyo wa kujitolea na kuonyesha kuwa msaada wa kijamii unaweza kubadilisha maisha ya mtu kwa kiwango kikubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *