Gossip

HUDDAH MONROE AWACHANA VILIVYO WANAUME WANAOTOKA KIMAPENZI NA WANAWAKE WENGI

HUDDAH MONROE AWACHANA VILIVYO WANAUME WANAOTOKA KIMAPENZI NA WANAWAKE WENGI

Mwanasosholaiti maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe ameamua kuwachana wanaume ambao hawawezi kutosheka na mwanamke mmoja.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Huddah amedai kwamba hawezi kufanya mapenzi na mwanamume ambaye ana mpenzi mwingine kwani kufanya hivyo ni kujidharau.

“Siwezi kufanya ngono na mwanaume ambaye ana mwanamke au mpenzi nyumbani kwake, siwezi fikiria kutoheshimika huko, wengi wenu mna nguvu kama hiyo mimi sina.” amesema.

Kulingana na Huddah wanaume wengi wakiwa wadogo hawajawahi kuonyeshwa upendo wa kweli, huku hisia zao zikiumizwa.

Mrembo huyo amesema wanaume wengi haswa Waafrika hawajahi pendwa vizuri wakati walipokuwa wadogo, ndio maana huwa wanalala na wanawake wengi ili kuthibitisha uwanaume wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *