
Msanii wa Bongofleva Ibraah ametangaza rasmi jina la album yake mpya ambalo ni “THE KING OF NEW SCHOOL”.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ibraah ameweka wazi kwamba iko tayari ingawa hajataja nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake hiyo.
Hii inaenda kuwa ni album ya kwanza kwa Ibraah tangu aanze safari yake ya muziki wake.
Nyota huyo ambaye alitambulishwa na lebo ya Konde Music Worldwide Aprili 11, mwaka wa 2020 ameshaachia EP moja iitwayo “STEPS” yenye jumla nyimbo 5 za moto.