
Mtandao wa Instagram unatarajiwa kuweka uwezo wa kupost kwa kutumia tovuti ya Instagram katika kompyuta. Watumiaji wa kompyuta watakuwa na uwezo wa ku-upload videos na picha katika akaunti za Instagram kwa kupitia website ya Instagram.
Hii ni feature ambayo watu wengi sana wanaihitaji hasa Account Managers na watu ambao wanatumia kompyuta katika shughuli mbalimbali. Badala ya ku-copy content kwenye simu ili utumia app ya Instagram katika simu, watu watakuwa na uwezo wa kutumia kompyuta kupost Instagram.
Feature hii imechelewa sana kuwekwa kwa kampuni ya facebook imekuwa iki-promote app ya Instagram. Facebook imekuwa na full-features katika tovuti yake lakini bado haikuweka feature ya kupost katika tovuti ya Instagram.
Feature hii inaanza kutoka wiki hii kwa baadhi ya watumiaji ila itatoka taratibu kwa watumiaji wote wa tovuti ya Instagram.