Instagram Yaleta Mabadiliko Mapya ya Reels kwa Urahisi Zaidi wa Watumiaji
Kampuni ya Instagram imeanzisha maboresho mapya kwenye kipengele chake cha Reels, yakilenga kuboresha uzoefu wa mtumiaji wakati wa kutazama video fupi. Mabadiliko haya mapya yanahusu namna ya kusimamisha (pause) na kuchezesha (play) video kwa urahisi zaidi. Kupitia sasisho hili jipya, watumiaji wa Instagram sasa wataweza kusimamisha au kuendelea na Reels kwa kubonyeza skrini mara moja tu. Hii inaleta urahisi na ufanisi zaidi, hasa kwa wale wanaopenda kudhibiti video kwa haraka bila usumbufu. Hapo awali, kipengele cha kubonyeza mara moja kilikuwa kinatumika kuzima sauti (mute). Hata hivyo, katika maboresho haya mapya, kazi hiyo imehamishwa sasa kuna kitufe maalum pembeni ya video kitakachotumika kuzima au kuwasha sauti. Mabadiliko haya yanaonyesha jinsi Instagram inavyoendelea kuboresha huduma zake ili kushindana na majukwaa mengine na kutoa uzoefu bora zaidi kwa watumiaji wake duniani kote.
Read More