
Mtandao wa Instagram umetangaza kuunganisha IGTV (video ndefu) na video za Feeds (video za posts za kawaida) ambapo zote zitaitwa Instagram Video.
Instagram imeondoa jina la IGTV na video ndefu zitabaki kama kawaida lakini hazitaitwa IGTV. Video za feeds ambazo huwa na urefu wa sekunde 60, zote zitaitwa Instagram Video huku Reels zikibaki kuwa video fupi ambazo zitakuwa na style ya video za TikTok.
Katika profile za watumiaji wa Instagram, itabaki tab ya Feeds ambayo itakuwa na posts za picha, Reels, na Instagram Videos na app ya IGTV itaitwa Instagram TV.
|