
Instagram inaweka mfumo wa kuhakiki akaunti mpya ambazo zinafunguliwa na akaunti ambazo Algorithm itahisi ni bot au Spam Account. Mfumo mpya utamhitaji mtumiaji mpya kujirekodi video fupi ya Selfie, ambayo inatumwa na kukaguliwa kama anayefungua akaunti ni mtu na sio robot.
Instagram itaanza utaratibu huo ili kuzuia akaunti hewa na Spam katika Instagram. Mfumo mpya unakuhitaji ujirekodi video ukigeuza uso kwenda upande wa juu, chini, kulia na kushoto; ili uso uonekane kisha mfumo utahakiki kama kweli ni mtu. Meta imesema video hiyo itahakikiwa na kuhifadhiwa kwa siku 30; na hazitumiki katika kukusanya Biometric Data.
Mfumo huu tayari unatumika sana na app za Tinder na Bumble ambazo zinatumia na picha kuhakiki mmiliki wa akaunti. Pia katika Wallets na Exchange za Crypto zinatumia picha ya Selfie na Kitambulisho au Passport kuhakiki kama kweli mmiliki wa akaunti ni mtu na sio robot au bot (Identity Verification).
Kwa Instagram sidhani kama watu wengi watapenda huu utaratibu!