Tech news

Instagram Yazindua App Rasmi kwa Watumiaji wa iPad

Instagram Yazindua App Rasmi kwa Watumiaji wa iPad

Instagram imetangaza rasmi kuanzisha programu maalum kwa watumiaji wa iPad, hatua inayokuja baada ya zaidi ya miaka 15 ya huduma hiyo kupatikana kwa watumiaji wa simu pekee. Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2010, Instagram haijawahi kuwa na toleo rasmi kwa iPad, hali iliyowalazimu watumiaji kutumia app ya iPhone ambayo haikuwa na muonekano unaoendana na skrini kubwa ya iPad.

Katika toleo hili jipya, Instagram imefanya mabadiliko kadhaa ya kimtindo na kimuundo. Ukurasa wa mwanzo wa app ya iPad umejikita zaidi kwenye maudhui ya video fupi (Reels) badala ya picha na machapisho ya kawaida (Feeds), tofauti na ilivyo kwenye toleo la simu. Aidha, sehemu ya maoni sasa inaweza kusomwa bila kuvuruga uonyeshaji wa video, na watumiaji wataweza kufungua ujumbe wa moja kwa moja huku wakiendelea kuona orodha ya mazungumzo yao upande mwingine wa skrini.

Ripoti za hivi karibuni zinaonesha kuwa watoto na vijana wengi hutumia iPad kwa matumizi ya burudani, hasa kupitia TikTok, ambayo tayari imewekeza katika matumizi ya iPad na Smart TV. Hatua ya Instagram kuzindua toleo hili inatazamwa kama njia ya kuingia rasmi kwenye ushindani wa jukwaa la maudhui ya video, likiwa linalenga kuvutia kundi hilo la watumiaji na kuongeza muda wa matumizi kwenye jukwaa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *