Tech news

Instagram Yazindua Kipengele Kipya cha Folders Katika DM

Instagram Yazindua Kipengele Kipya cha Folders Katika DM

Instagram imeanza kuweka sehemu mpya inayowezesha watumiaji kuongeza folders katika upande wa ujumbe wa moja kwa moja (DM). Hatua hii inalenga kurahisisha upangaji na upatikanaji wa ujumbe, hasa kwa wale wanaopokea jumbe nyingi kila siku.

Kupitia maboresho haya, watumiaji sasa wanaweza kutenganisha jumbe kwa urahisi kulingana na makundi tofauti. Mfano, mtu anaweza kutenganisha jumbe za waliyojibu kupitia Instagram Stories, kuweka tofauti kati ya jumbe kutoka kwa Followers na wale ambao si Followers, kutenga jumbe za kibiashara, pamoja na jumbe kutoka kwa akaunti zilizo na alama ya kuthibitishwa (verified).

Kipengele hiki kinatarajiwa kuwasaidia sana wafanyabiashara, wabunifu wa maudhui na watumiaji wenye ufuasi mkubwa ambao mara nyingi hukumbwa na changamoto ya kusimamia mawasiliano mengi kwa wakati mmoja.

Kwa sasa Instagram inalisambaza kipengele hiki hatua kwa hatua, na katika muda mfupi ujao watumiaji wote duniani wataweza kufurahia urahisi huu mpya wa kusimamia ujumbe wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *