Tech news

Instagram yazindua kipengele kipya cha kuchora ndani ya DM

Instagram yazindua kipengele kipya cha kuchora ndani ya DM

Kampuni ya Instagram imeweka mabadiliko mapya katika sehemu ya Direct Messages (DM), ambapo sasa watumiaji wote wanaweza kuchora moja kwa moja kwenye skrini ya mazungumzo.

Kupitia mfumo huu mpya, mtumiaji anaweza kuchora au kuandika kwa mkono katika sehemu yoyote ya skrini ya DM, na mtu anayewasiliana naye ataweza kuona michoro hiyo papo kwa papo, bila kuchelewa.

Kipengele hiki kipya kinapatikana kupitia alama ya (+) iliyopo chini ya skrini ya mazungumzo. Baada ya kubonyeza alama hiyo, mtumiaji ataona chaguo jipya lenye jina “Draw”, ambalo linamruhusu kuchora au kuandika alivyotaka moja kwa moja ndani ya DM.

Instagram imesema maboresho haya yamelenga kuongeza ubunifu na njia za kujieleza kwa watumiaji wake, sambamba na kuboresha uzoefu wa mawasiliano binafsi.

Kipengele hiki kinatarajiwa kuwafikia watumiaji wote duniani katika hatua za awali za masasisho mapya ya programu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *