Mtandao maarufu wa kijamii Instagram umezindua kipengele kipya kinachowezesha watumiaji kudhibiti Follow Requests kutoka kwa akaunti ambazo tayari wanafuata. Kipengele hiki kinakusudia kurahisisha njia ya kudhibiti nani anayeweza kujiunga na mtiririko wa watumiaji, na kutoa udhibiti zaidi juu ya faragha ya akaunti.
Kwa kutumia sehemu hii mpya, mtumiaji wa Private Accounts anaweza kukubali Requests kutoka kwa akaunti ambazo tayari wanazi-follow, bila taabu ya kukagua kila moja..
Kwa mfano, kama kuna akaunti ambayo unai-follow, akaunti hiyo inaweza kuku-follow automatically bila wewe kupata taabu ya kuiruhusu, mradi tu akaunti yako ni private. Kipengele hiki kinasaidia okoa muda na kurahisisha usimamizi wa Follow Requests, huku kikiweka watumiaji kwenye udhibiti zaidi wa faragha yao.
Hatua hii inakuja wakati Instagram inajitahidi kuongeza udhibiti wa faragha na kutoa uzoefu bora zaidi kwa watumiaji wake duniani kote.