Entertainment

INVISIBLE CURRENCY ALBUM YA KHALIGRAPH JONES YAWEKA REKODI BOOMPLAY KENYA

INVISIBLE CURRENCY ALBUM YA KHALIGRAPH JONES YAWEKA REKODI BOOMPLAY KENYA

Rapa Khaligraph Jones anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Album yake ” Invisible Currency ” ambayo tayari ina takriban wiki moja tangu itoke rasmi.

Goods ni kwamba Album ya “Invisible Currency” imefanikiwa kufikisha jumla ya Streams million moja kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya.

Kupitia Instagram page yake Papa Jones amewashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia album yake ya Invisible Currency huku akiwataka waendelea kuisikiliza album hiyo kwenye mtandao wa Boomplay Kenya.

Album ya “Invisible Currency” iliachiwa rasmi Machi 7 mwaka 2020 ikiwa na jumla ya ngoma 17 ya moto na ni album ya pili kwa mtu mzima  Khaligraph Jones  tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Testimony 1990 iliyotoka mwaka 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *