
Mwanamitindo na mjasiriamali maarufu nchini Kenya Huddah Monroe, ameweka wazi kuwa yuko tayari kuwa mama ikiwa mwanamume anayetamani kupata naye watoto ataweka mezani kitita cha $1,000, 000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi millioni 113 za Kenya.
Huddah ameweka wazi kuwa atakuwa tayari kuwa mama kwa mwanamume anayetamani kupata naye watoto endapo ataweka mezani kiasi hicho cha pesa na kuweka wazi kuwa kuhusu malezi/msaada wa mtoto watakubalina wakati wa kushiriki tendo ili kupata mimba.
Kupitia instastory kwenye mtandao wa Instagram Huddah Monroe ameadika ujumbe unaosomeka βNauza tumbo langu. Lol! $1, 000, 000 ili niwe mama wa mtoto wako mchanga. Kuhusu Msaada wa mtoto tutakubalina wakati wa kushiriki tendo ili kupata mimba,β
Mnamo mwaka 2020, Huddah alikiri kwamba kamwe hatoweza kumhifadhi kwenye tumbo lake mtoto wa mwanamume fukara,.