Msanii wa muziki nchini Kenya, Iyanii, amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa alikataa ofa nono ya shilingi milioni 3 kutoka kwa mwanamke aliyekuwa akitaka kuvunja ubikra wake.
Akizungumza kwenye Mic Check Podcast, Iyanii amesema tukio hilo lilianza mwanamke huyo alipomfuata kwa ofa ya awali ya shilingi laki tano. Hata hivyo, baada ya yeye kukataa, mwanamke huyo aliongeza dau hilo hatua kwa hatua hadi kufikia shilingi milioni 3, akijaribu kumbadilisha msimamo wake.
Hitmaker huyo wa Donjo Maber, ameeleza kuwa licha ya kiwango kikubwa cha pesa kilichotolewa, alisimama kidete na kushikilia uamuzi wake wa kuchunga ubikra wake, akisema misingi na maamuzi yake binafsi ni muhimu zaidi kuliko tamaa ya mali.
Iyanii pia amekiri kuwa madai yake yamekuwa yakizua mshangao kwa wengi, huku baadhi ya watu wakionyesha kutokuamini. Hata hivyo, amesema yeye binafsi anajijua vyema, akisisitiza kuwa hajawahi kushiriki mapenzi na mwanamke yeyote katika miaka yote 27 ya maisha yake.