Msanii nyota wa muziki wa Kenya, Iyanii, ameonyesha hisia zake baada ya kupuuzwa na waandaaji wa matamasha licha ya kuwa na nyimbo nyingi zilizovuma.
Kupitia ujumbe wake, Iyanii amesema kuwa ni haki yake kama msanii kupata nafasi sawia na wengine, akieleza kuwa ni jambo lisilo la haki kuachwa nje ya matukio makubwa ya burudani.
Hata hivyo, msanii huyo wa ngoma ya Donjo Maber amesema hatakata tamaa, akisisitiza kuwa anaamini muziki wake utazungumza kwa niaba yake na kuthibitisha thamani yake katika tasnia ya burudani.
Kauli ya Iyanii imekuja baada ya mashabiki wake kuzindua kampeni mtandaoni iitwayo “Justice for Iyanii”, wakilalamikia namna waandaaji wa matamasha wanavyompuuza msanii huyo licha ya mafanikio yake makubwa.
Mashabiki hao wamesema kuwa ni unyanyapaa na upendeleo unaoendelea katika sekta ya muziki, kwani Iyanii ameachia nyimbo nyingi zilizotamba katika kipindi cha mwaka moja uliopita, lakini bado hajapewa nafasi kwenye matamasha makubwa nchini Kenya.