
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Jason Derulo anadaiwa kuwashambulia watu wawili baada ya watu hao kumwita jina la “Usher”
Kwa mujibu wa TMZ wameripoti kuwa tukio hilo limetokea kwenye Hoteli moja huko Las Vegas nchini Marekani.
Mashahidi wanasema kuwa mtu mmoja alimwita Jason kwa jina la Usher jambo ambalo lilimchukiza staa huyo na kuanza kumshambulia kwa kumpiga ngumi ya uso mtu huyo kisha kuhamia kwa mtu mwingine na kumshambulia pia.
Mpaka sasa watu hao hawajafungua mashitaka yoyote dhidi ya staa huyo lakini inawezekana huko mbeleni wakafungua mashtaka endapo wakibadili mawazo yao. Pamoja na kujeruhiwa huko watu hao hawajaenda hospitali yoyote kupata hata huduma ya kwanza