
Rapa mkongwe kutoka nchini Marekani Jay Z amefunguka kuhusu VERZUZ na kujigamba kwamba hakuna msanii yeyote ambaye anaweza kusimama na kushindana naye kwenye Jukwaa hilo.
Kupitia Twitter Spaces ambayo iliwakutanisha pamoja na Alicia Keys na wadau wengine wa muziki kujadili kuhusu album mpya ya Alicia Keys ‘KEYS’ Jay-Z alisikika akisema “Hakuna wa kusimama/kushindana na mimi kwenye Jukwaa la Verzuz. Siwezi kudanganya, na wala simkosei mtu yeyote heshima. Kila mmoja ni mkali, wamefanya kile walichofanya. Hakuna wakusimama na mimi kwenye ile steji. Hakuna nafasi hiyo kamwe kwamba mtu yeyote kusimama na mimi kwa muda wa masaa mawili, haiwezi kutokea kamwe.” alifunguka na kupigilia msumari pia kwamba hatokuja kushiriki Verzuz.
Hivi karibuni rapa Rick Ross alitangaza uwezekano wa kusimama na Jay-Z na kushindana naye kwenye Jukwaa la Verzuz.