
Rapa kutoka Marekani Jay-Z ametajwa kuhusika kwenye mpangilio wote wa onesho la Rihanna kwenye Halftime show ya Super Bowl ambayo itafanyika Februari 12, mwaka 2023.
Jay-Z ambaye alimsaini Riri kwenye label ya Def Jam mwaka 2005, alianza kuihudumia NFL kwenye sekta ya burudani tangu mwaka 2019 ambapo kwenye utawala wake alifanikiwa kuangusha performance kubwa ya Kihistoria mwaka 2022 kwa kuwaleta pamoja, Dr. Dre, Mary J. Blidge, Kendrick Lamar, Snoop Dogg, Eminem na 50 Cent.