
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Jennifer Lopez amefunguka kwamba ilibaki kidogo aachane na muziki kutokana na watu kuzungumzia sana mahusiano yake na kumkosoa sana kuhusu mwili wake.
Kwenye Documentary yake mpya “Halftime” ambayo imeanza kuruka kupitia Netflix, Jennifer Lopez amesema muziki wake ulifunikwa na maneno ya watu ambao walikuwa wakimkosoa kwa mengi ikiwemo kukosa makalio makubwa lakini pia kuwa kwenye mahusiano na wanaume tofauti tofauti katika kipindi kifupi.
“Nimekulia kwenye mazingira ya Wanawake wenye shape kubwa, hivyo sikuwa na chochote cha kuhofia. Lakini ilikuwa ni ngumu pale unapofikiria watu wanakuona kama kituko. Licha ya yote niliyofanikiwa, hamu yao kuandika stori kuhusu maisha yangu binafsi, kulifunika (Overshadowed) kila kitu kilichotokea kwenye maisha yangu ya muziki. Walikuwa wakisema kwamba Mimi sio mwimbaji mzuri, wala sio mwigizaji mzuri, sio mnenguaji mzuri, sikuwa mzuri kwa chochote na wala sikustahili kuwa hapa.” alikaririwa Jennifer Lopez.