
Mwimbaji nyota wa muziki wa Injli nchini Tanzania, Joel Lwaga ameshinda tuzo za Maranatha zilizotolewa huko Pennsylvania, nchini Marekani.
Tuzo hizo ambazo zimefanyika mwishoni mwa wikiendi katika ukumbi wa Grand Gala na kuhudhuruwia na mamia ya watu wakiwemo wadau wa neno la Mungu na waimbaji wenyewe, iliwakutanisha miamba mbalimbali wa tasnia hiyo katika vipengele mbalimbali.
Joel lwaga ambaye ameiwakilisha vyema Afrika Mashariki kwenye tuzo hizo katika msimu wake huu wa tatu, ameshinda kwenye kipengele cha (Male Minister Of Excellence).
Sanjari na hilo, kwasasa Joel Lwaga yupo mbioni kuachia album yake mpya ambayo itaingia sokoni rasmi tarehe 1 mwezi ujao