
Mkongwe wa muziki nchini uganda Jose Chameleone amehapa kukuza muziki wa msanii Allan Hendrick kwani ni kijana ambaye ana ari ya kutaka kufanya makubwa kwenye muziki wake.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Bosi huyo wa leone island amemwagia sifa msanii huyo chipukizi kwa kumtabiria mema kuwa atakuja kuwa msanii mkubwa kwenye kiwanda cha muziki nchini uganda kutokana na kipaji chake cha kipekee katika muziki wake.
Kauli ya Chameleone imekuja mara baada ya kuonekana katika siku za hivi karibuni akitumia muda wake mwingi kukaa na Allan Hendrick ambaye ni kijana wa msanii mwenzake Bebe Cool.
Utakumbuka msanii Bebe cool amekuwa akikosolewa na watu kwa kutompa support kijana wake Allan Hendrick kutokana na hatua yake ya kumuacha akipambana mwenyewe kwenye muziki wake licha ya bebe cool kumiliki lebo ya muziki ya Gagamel ambayo ina uwezo wa kukuza kipaji cha msanii huyo.