
Mwanamuziki Jose Chameleone amewatolea uvivu watu wanaopenda kufanya mazoezi akiwataja kuwa ni wavivu ambao hawana chochote cha kufanya maishani mwao.
Akiwa kwenye moja ya Interview Chameleone anasema aliwahi kwenda gym lakini aligundua kuwa alikuwa anapoteza muda wake mwingi, na hivyo akaamua kuacha.
Hitmaker huyo wa “Baliwa” amesema alihamua kuwekeza muda wake katika kufanya kazi, na hiyo imemsaidia kupata kipato kizuri ambacho kinamsaidia kufanikisha baadhi mambo yake.
Hata hivyo Chameleone anasema anarithika na muonekano wake kimwili ingawa kuna baadhi ya watu wanadai hana mwili wa masupastaa.
Kwa upande mwake, msanii Bebe Cool anaamini kuwa mwanamuziki anahitaji kufanya mazoezi ili awe na muonekano mzuri kwa mashabiki wake.