LifeStyle

Jovial Afunguka Sababu ya Kutoanika Mtoto Wake Mitandaoni

Jovial Afunguka Sababu ya Kutoanika Mtoto Wake Mitandaoni

Mwanamuziki maarufu wa Kenya, Jovial, amefunguka kuhusu uamuzi wake wa kutoweka sura au jina la mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instastori, Jovial alisema kuwa hatua hiyo ni njia yake ya kumlinda mtoto wake dhidi ya madhara ya maneno na mitazamo hasi inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii. Alisisitiza kuwa, kama mzazi, jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha usalama na utulivu wa mtoto wake.

Kauli yake ilikuja baada ya shabiki mmoja kumuuliza kwa nini hadi sasa hajawahi kushirikisha mashabiki taarifa zozote kumhusu mtoto wake, tofauti na mastaa wengine ambao huanika familia zao hadharani.

Jovial ameungana na orodha ya wasanii na watu mashuhuri ambao huchagua kutokuweka wazi maisha ya watoto wao, wakiamini kuwa faragha ni kinga muhimu katika ulimwengu wa kidijitali wenye changamoto nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *