Gossip

JOVIAL AKOSHWA NA SHABIKI ALIYECHORA TATTOO YENYE JINA LAKE MKONONI

JOVIAL AKOSHWA NA SHABIKI ALIYECHORA TATTOO YENYE JINA LAKE MKONONI

Female singer kutoka Kenya Jovial amefurahishwa sana na kitendo alichofanyiwa na shabiki wake kwa kujichora Tatoo yenye jina lake mkononi.

Kulingana na screen shots za ujumbe alizotumiwa na shabiki yake mmoja, Binti huyo aliyefanya hivyo hajawahi kukutana na jovial wala hawajawahi hata kuongea nae ila aliamua kucchora tattoo ya jina la msanii huyo kama njia ya kumuonyesha upendo kwani anazikubali nyimbo zake.

Hata hivyo jovial ameshindwa kuficha furaha yake kwa shabiki huyo ambapo amewataka watumiaji wa  mitandao ya kijamii wamsaidie kumtafuta mrembo huyo ili aweze kukutana nae kwani amekoshwa na upendo ambao alimuonyesha kwa kuchora tattoo yenye jina lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *