
Msanii kike nchini Jovial ametoa onyo kwa mashabiki zake ambao kwa njia moja au nyingine wana mpango wa kumdhalalisha kijinsia akiwa jukwaani.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram msanii huyo amesema kuanzia sasa atakuwa anapambana moja kwa moja na shabiki atakayejaribu kumshika vibaya akiwa jukwaani anatambuiza huku akisisitiza kuwa atamshushia kichapo kabla walinzi wake awajaingilia kati
Kauli yake Jovial imekuja mara baada ya shabiki yake mmoja wikiendi hii iliyopita kwenye performance kumvamia akiwa jukwaani na kumshika makalio pasi na idhini jambo ambalo lilimfanya kusitisha show yake kwa muda.
Hata hivyo mashabiki walionekana kwa kughabishwa na kisa hicho ambapo wamewataka waandaji wa matamasha ya muziki kuwapa ulinzi wa kutosha wasanii wanapoalikwa kufanya shows kwenye matamasha yao