
Mwanamuziki nyota nchini Jovial amefunguka sababu ya kutoshirikiana na wasanii wa kike kwenye kazi zake za muziki.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Hitmaker huyo wa “Mi Amor” amesema kuwa wasanii wengi wa kike ni wanafiki na ndio maana amekuwa akifanya kolabo nyingi na wasanii wa kiume.
Jovial amedai kwamba anapendelea sana kuwa na marafiki wa kiume kwa sababu ni watu ambao wana moyo wa kusaidia tofauti na wanawake huku akisema ubinafsi ambao wasanii wa kike wanao kwenye shughuli zao ndio imechangia muziki wa Kenya kuwa na wasanii wachache wanawake.