
Rapa Juliani amewapa somo wasanii chipukizi wanaolaza damu kwenye suala la kuupeleka muziki wao kwenye kiwango kingine.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Juliani amesema wasanii hao wanapaswa kuchangamkia fursa zilizopo badala ya kulalamika kila mara kuwa wametengwa na jamii inayowazunguka.
“Usijidharau msee, because when I look at my career, from where I started to now my fourth album, and the amazing things I’ve done so far, the only constant thing ni nilikuwa najichocha. I had no clue what I was doing but I had the courage to listen to that voice and the courage to boldly take that step.”
“Kuna a certain point mtu hufika kwa career when you think you need to do certain things to fit in… but after four-five years of connecting with people I realised kumbe I was contributing to that space just by being myself!” Amesisitiza
Hata hivyo amewashauri wasanii wasiongoje wahamasishwe na watu wengine na badala yake wasipambanie ndoto zao wenyewe bila kukataa tamaa hadi pale watakapofanikisha malengo yao.
“Sikupatii collabo, una ufala! That’s what everybody [starting out] asks for. Ati ‘Nirushie kacollabo’… No. You have what it takes, I only know about mine, I don’t know about yours,” alimalizia