Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Jux na mkewe kutoka Nigeria, Priscilla Ojo,wameibua msisimko mkubwa mtandaoni baada ya kudokeza mipango yao ya kuhamia nchini Kenya na kununua makazi mapya.
Tetesi za wawili hao kuhama zilianza kusambaa baada ya kushiriki picha zenye mvuto na video fupi wakiwasili kwenye jumba la kifahari jijini Nairobi. Kitendo hicho kilizua uvumi na minong’ono mingi kuhusu hatua yao kubwa inayofuata kimaisha.
Kuongeza chumvi kwenye habari hizo, kampuni ya usanifu wa mambo ya ndani ya Fine Urban Construction & Interiors pia ilichapisha picha za siri za jumba hilo la kifahari ambalo inadaiwa wawili hao wanalimezea mate.
Hatua hii imefurahisha mashabiki wao, ambao sasa wanangoja kwa hamu kuthibitishwa rasmi kwa uamuzi huo wa Jux na Priscilla kuhamishia makazi yao makuu nchini Kenya.