Gossip

Juma Lokole Asema Ritha Hana Mvuto wa Kumfanya Diamond Kumuacha Zuchu

Juma Lokole Asema Ritha Hana Mvuto wa Kumfanya Diamond Kumuacha Zuchu

Mdau wa burudani Juma Lokole amtolea uvivu mrembo Ritha, akisema hana uwezo wa kuvunja uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond Platnumz na Zuchu.

Akizungumzia sakata hilo, Juma Lokole amesema wazi kuwa Ritha hana uzuri wala mvuto wa kumfanya Diamond kumuacha Zuchu, akisisitiza kuwa penzi la wawili hao lipo imara na halitetereki kwa tetesi au maneno ya mitandaoni.

Lokole amedai kuwa endapo Ritha anadhani kuvujisha sauti au taarifa zinazodaiwa kumhusisha na Diamond kunaweza kuharibu au kusambaratisha mahusiano ya wawili hao, basi ajue hilo halitowezekana.

Aidha, Juma Lokole amemwonya Ritha kuacha tabia ya kuvujisha sauti au siri za watu, akisema mwenendo huo unaweza kumharibia mustakabali wa mahusiano yake, kwani wanaume wengi wanaweza kumuogopa kwa kuhofia siri zao kuwekwa hadharani.

Kauli ya Juma Lokole imekuja baada ya Ritha ambaye anadaiwa kutoka kimapenzi na Diamond kumtolea Diamond na Zuchu maneno mazito, ambapo alienda mbali zaidi na kudai Diamond amekuwa akimtaka kimapenzi kwa siri na hata kuwatuma baadhi ya ndugu zake kumshawishi ili warudiane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *