Mdau wa masuala ya burudani, Juma Lokole, amezua mjadala mpana mitandaoni baada ya kudai kuwa Wema Sepetu aliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mfanyabiashara tajiri anayefahamika kwa jina la MO.
Akizungumza kupitia Instagram yake, Juma Lokole amesema licha ya madai hayo, Wema aliweza kuficha siri za mahusiano yake na hakuwahi kuanika mambo ya ndani hadharani, hali ambayo imemsaidia kulinda heshima yake katika jamii.
Kutokana na hilo, Juma Lokole amemtaka Rita, Mrembo anadaiwa kutoka kimapenzi Diamond, kuiga mfano wa Wema Sepetu kwa kuacha tabia ya kusambaza siri za mahusiano mitandaoni. Amesema badala ya kelele na lawama, Rita anapaswa kutumia fursa anazopata katika mahusiano kujijenga kiuchumi na kimaendeleo.
Kwa mujibu wa Juma Lokole, mahusiano yanaweza kuwa daraja la kuboresha maisha ya wanawake endapo yatatumika kwa busara, nidhamu na hekima, huku akisisitiza kuwa kuanika siri hadharani kunaharibu taswira ya mwanamke na kunapunguza fursa za wanaume kumchumbia.