Sports news

Junior Stars Yalaza Rwanda 2-1 Kwenye Michuano ya CECAFA

Junior Stars Yalaza Rwanda 2-1 Kwenye Michuano ya CECAFA

Timu ya taifa ya soka ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Stars, ilitoka nyuma na kuandikisha ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda, katika mchuano wao wa kundi A kuwania ubingwa wa taji ya CECAFA kwa wachezaji wasiozidi umri wa m,iaka 17 inayoendelea nchini Ethiopia.

Rwanda ilifunga bao la kwanza na kuchukua uongozi mnamo dakika ya 37 kupitia kwa Nshimiyimana Olivier. Hata hivyo, Junior Stars ilijibidiisha katika kipindi cha pili na kubatlisha matokeo hayo.Nicholas Ochola alisawazisha dakika ya 69, kisha Trevor Nasasiro akafunga bao la ushindi dakika ya 77 na kuipa Kenya ushindi huo muhimu.

Matokeo hayo yanaiweka Junior Stars katika nafasi ya pili kundini A. Kenya  sasa itachuana na South Sudan katika mechi yake ijayo jumatatu kisha ihitimishe michuano yake ya makundi dhdi ya wenyeji Ethiopia alhamisi Novemba 27.

Timu mbili zitakazomaliza katika za mwanzo zitajikatia nafasi ya kushiriki katika fainali za komb la bara afrika kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *