
Mwimbaji wa nyimbo za injili Justina syokau amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa alizawadiwa gari iliyokuwa imetumika kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake.
Kupitia mitandao yake ya kijamii amesema hatotishwa na maneno ya walimwengu huku akisisitiza kuwa ana furaha mwaka 2023 umeanza vyema kwa zawadi ya nguvu kutoka kwa mpenzi wake.
“Aaaa am happy I have a new car Tena present sijanunua nimepewa nashukuru sana . Kama kuna kitu
sio mpya sijui, kama kuna kitu mpya mzee sijali what I am happy about is Nimepanuliwa mipaka”
“maadui awajafurahi sio vibaya nataka nipeleka maaadui roadtrip mpaka mwezi wa sita,” Aliandika.
Kauli ya Justina imekuja mara baada ya wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa gari aina ya Land Cruiser V8 aliyopewa na mchumba wake kama zawaidi kwenye siku yake ya kuzaliwa sio jipya.
Justina Syokau aligonga vichwa vya habari nchini mwaka 2022 alipowadanganya wafuasi wake kuwa alitumia shilling million 2 kufanya upasuaji wa kuongeza makalio yake, madai ambayo yalikuja kubainika kuwa ilikuwa ni njia ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni.
Kitendo hicho kiliwafanya walimwengu kutoamini, matukio ya mwanamama huyo mtandaoni wakimtaja kuwa mpenda kiki.