Entertainment

KAA LA MOTO AACHIA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

KAA LA MOTO AACHIA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

Rapa kutoka Kenya Kaa la Moto ameanika hadharani tracklist ya Album yake mpya inayokwenda kwa jina la Leso ya Mikatilili.

Kupitia Instagram yake Rapa huyo amechapisha artwork ya Album hiyo ambayo ina jumla ya ngoma 12 ya moto huku ikiwa na kolabo 10 pekee.

Kaa La Moto amewashirikisha wakali kama Masauti, Hart the Band, Chikuzee, Mercury, Kigoto, Iddi Singer, Lavido,Escobar, huku Album yenyewe ikiwa na nyimbo kama Nipe Mji, Sisikii Sauti, Karibu mwanangu na nyingine nyingi.

Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea Leso ya Mikatilili Album  ambayo itapatikana Exclusive kupitia mtandao wa Boomplay Kenya licha kutoweka wazi tarehe ambayo album hiyo itaingia sokoni.

Hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwa mtu mzima Kaa La Moto baada ya kesi ya mwaka wa 2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *