Mpenzi wa Harmonize, Kajala Masanja, ametoa onyo kali kwa mabinti kuhusu aina ya wanaume wanaopaswa kuwaepuka kwenye mahusiano.
Kupitia Instastory yake, Kajala amewataka mabinti kuwa makini sana na wanaume wasiotoa msaada wa kifedha kwa wenza wao. Kwa mujibu wa Kajala, mwanaume anayeshindwa au kukataa kumpatia mwanamke hela ya matumizi ni ishara ya hatari katika mahusiano.
Mrembo huyo amedai kuwa mwanamke anapaswa kaa mbali na mwanaume wa aina hiyo, akisisitiza kuwa msaada wa kifedha ni sehemu ya uwajibikaji katika uhusiano wa kimapenzi.
Hata hivyo, ujumbe wake umeonekana kuwalenga mabinti wengi wanaokumbwa na changamoto katika mahusiano, akiwahimiza kujithamini na kuchagua wenza wanaothamini na kuwajibika ipasavyo.