Gossip

Kajala Masanja Afichua Alivyohongwa Mamilioni na Wanaume

Kajala Masanja Afichua Alivyohongwa Mamilioni na Wanaume

Muigizaji nyota wa filamu za Bongo, Kajala Masanja, amekiri hadharani kuwa alihongwa mamilioni ya fedha na wanaume waliotaka kutoka naye kimapenzi kipindi ambacho nyota yake ilikuwa imeng’aa kwenye tasnia ya filamu.

Akizungumza kupitia podcast ya A List Stars, Kajala amesema licha ya kupata pesa nyingi kutoka kwa wanaume tofauti hakufanya jambo la maana zaidi ya kula bata.

Kajala amesema hakuna mwanaume anayeweza kumshtua kwa kumhonga kwa sababu tayari alishapokea kiasi kikubwa cha fedha miaka ya hapo nyuma.

Kauli yake iliungwa mkono na mastaa wenzake waliokuwa naye kwenye kipindi hicho, akiwemo Irene Uwoya, Jackline Wolper na Aunt Ezekiel, ambao wamekiri kuwa hali kama hiyo ni ya kawaida kwa mastaa wa kike katika tasnia ya filamu na burudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *