
Mwanamuziki wa dancehall kutoka nchini Uganda Kalifah Aganaga amesikitishwa na kitendo cha Catherine Kusasira kuangua kilio hadharani kwenye mahojiano yake hivi karibuni kutokana na ugumu wa maisha.
Kwenye mahojiano na Spark TV, Aganaga amesema ni aibu kwa mwanamuziki huyo mkongwe kujidhalalisha mbele ya umma kama mtoto ikizingatiwa kuwa alitumia vibaya mshahara aliokuwa analipwa na serikali kipindi anahudumu kama mshauri wa rais Yoweri Museveni.
Kauli ya aganaga inakuja mara baada ya catherine kusasira kunukuliwa akieleza masaibu kuwa tangu atemwe kama mshairi wa rais mwaka wa 2021 amekuwa akipitia kipindi kigumu kiuchumi kiasi cha madalali kupiga mnada mjengo wake wa kifahari na gari yake aina Land cruiser V8 kwa ajili ya kukamilisha madeni anayodaiwa.