Entertainment

KAMBUA ATOA WITO KWA MASHABIKI KUWAOMBEA WALIOPOTEZA WATOTO WACHANGA

KAMBUA ATOA WITO KWA MASHABIKI KUWAOMBEA WALIOPOTEZA WATOTO WACHANGA

Mwimbaji wa nyimbo za injili Kambua amewahimiza mashabiki kuwaombea wale wote waliopoteza watoto wa changa kabla na baada ya kuzaliwa.

Kupitia instastory yake kweye mtandao wa Instagram ameandika ujumbe wa kuwataka wafuasi wake kuwaonyesha upendo kwa kuwapigia simu au kuwatumia ujumbe kama njia ya kuwafariji kuwa watoto wao wachanga waliotangulia mbele za haki wana dhamana kubwa.

Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa kitendo cha mzazi kumpoteza mtoto mchanga kabla na baada ya kuziliwa ni kichungu zaidi ambapo amefichua kuwa hivi karibuni atafunguka kwa kina kuhusu tukio la huzuni ambalo lilimtokea mwaka mmoja uliopita.

Utakumbuka Kambua mwaka 2021 alipoteza mtoto wake mchanga kwa njia ya tatanishi na tangu kipindi hicho hajawahi rejea katika hali yake ya kawaida kutokana na kuathirika kisaikolojia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *