Gossip

KANYE WEST ADAIWA KUMPIGA SHABIKI NGUMI, AANGUKA CHINI VIBAYA

KANYE WEST ADAIWA KUMPIGA SHABIKI NGUMI, AANGUKA CHINI VIBAYA

Januari 13 mwaka huu haikuwa siku nzuri kwa Kanye West, alionekana mtu mwenye hasira sana. Taarifa zinasema kwamba hakutaka kusogelewa na mtu yeyote yule kwa ajili ya kupiga picha wakati anashuka chini ya jengo la studio, Los Angeles.

YE alimaanisha, aliishia kumtwanga ngumi mbili jamaa mmoja ambaye alimfuata kupiga picha, ngumi ya kichwa na kisha ya shingo vilitosha kumuangusha chini shabiki huyo ambaye alibamiza kichwa chini baada ya kuanguka na kulala hapo hapo.

Kwenye video anaonekana Kanye West akizozana na binamu yake huku akimwambia “get away from me” Kanye alionekana mwenye hasira huku binamu yake akimsisitiza waite polisi kwa ajili ya kumuangalia shabiki yule.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *