Entertainment

Kanye West afunga ndoa ya siri na mfanyikazi wake

Kanye West afunga ndoa ya siri na mfanyikazi wake

Rapa kutoka Marekani Kanye West ameripotiwa kufunga ndoa tena baada ya kuachana na Baby Mama wake Kim Kardashian.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, YE amefunga ndoa na mwanamke aitwaye Bianca Censori ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yake ya Yeezy, akihudumu kama mbunifu wa usanifu yaani Architectural designer.

Mapaparazzi wa TMZ wamekinasa kidole cha YE kikiwa na Pete ya ndoa, ambapo inatajwa ndoa hiyo ilikuwa ya siri.

Mapema wiki hii Kanye West alionekana na mwanamke huyo ambaye alikuwa ametia nywele za blonde kichwani, wakipata chakula kwenye mgahawa mmoja mjini Beverly Hills.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *