
Staa wa muziki wa hiphop nchini Marekani Kanye West anaenda kuwa mtu asiye na makazi, ametangaza mpango wake wa kubadilisha nyumba zake zote kuwa Makanisa.
YE amefunguka hayo kwenye mahojiano na Jarida la Culture Magazine ambapo anukuliwa akisema “Nitageuza nyumba zangu zote kuwa makanisa pamoja na kutengeneza kituo cha watoto yatima ambacho kutakuwa eneo ambalo mtu yoyote ataweza kupata mahitaji yake ya muhimu na chakula kitakuepo muda wowote”.
Ikumbukwe Kanye West amekuwa akiongoza huduma ya Sunday Service, huduma ya kiroho ambayo hubadilisha nyimbo za kidunia kuwa nyimbo za kumsifu Mungu.