Entertainment

Kanye West aondolewa kwenye orodha ya mabilionea

Kanye West aondolewa kwenye orodha ya mabilionea

Muda mfupi baada ya kampuni ya Adidas kutangaza kuachana na rapa Kanye West, jarida la Forbes limeibuka na kutangaza kuwa rapa huyo ameondelewa rasmi kwenye orodha ya mabilionea kutokana na thamani yake ‘net worth’ kushuka.

Kanye West amejikuta akiingia katika wakati mgumu baada ya kutoa kauli za chuki dhidi ya jamii ya watu wa kiyahudi wiki kadhaa zilizopita, kitendo kilichopelekea kampuni mbalimbali kama Balenciaga na Adidas kuvunja naye mkataba.

Mikataba aliyoisani rapa huyo na makampuni mbalimbali makubwa duniani iliongeza thamani yake mpaka kufikia hatua ya kuwa Bilionea, lakini baada ya makampuni hayo kuachana naye thamani yake imeshuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *