
Mwanamuziki kutoka Uganda Kapa Cat, ametishia kumfungulia mashtaka promota mmoja huko Bugiri kwa madai ya kuwachochea mashabiki kuaharibu gari lake.
Kapa Cat amesema promota huyo anayefahamika kwa jina la Kim aliwaambie mashabiki kuwa hajafaki eneo la show jambo ambalo liliwafanya mashabiki kuzua vurugu na kuanza kuaharibu gari lake alilokuwa ameegesha karibu ukumbi wa burudani.
Hata hivyo amelaani tukio hilo kwa kusema kwamba show ya promota huyo ilikuwa mbovu kuwahi kuaandaliwa nchini uganda ambapo amedai anaelekea mahakamani kufungulia kesi  kwa kumsababishia hasara ikizingatiwa kuwa alikuwa amefika eneo la show mapema kwa ajili ya performance yake.